|
WA KWANZA KULIA NI MCH. EZEKIEL JOSEPH SANJARI NA MKEWE ANNA JOSEPH,picha na makiaba. |
Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha ewe mteule wa MUNGU wetu aliye mbinguni katika makala hii, ambayo inalenga kukujuza na kukuhabarisha njia kuu saba ambazo zitakusaidia kuimarisha mahusiano yako na MUNGU.
Ujumbe huu umetolewa leo madhabahuni katika kanisa la VICTORY CHURCH LA TAG lililopo hapa mkoani ARUSHA eneo la kwa MOROMBO na mwalimu EZEKIELI JOSEPH kutoka jijini DR ES-SALAAM, KARIBU SASA.
Mstari wa kusimamia.
ZAB 27:4 Neno moja nimelitaka kwa Bwana nalo ndilo nitakalolitafuta,nikae nyumbani mwa Bwana siku zote za maisha yangu niutazame uzuri wa BWANA nakutafakari hekaluni mwake.
1.Hatu ya kwanza [KWAME USIPOTEZE NJAA NA KIU YAKO KWA MUNGU,
Usimkinai MUNGU wala kumuona kama hana umuhimu,kwani adui akifanikiwa kuipoteza kiu na njaa hiyo atakupoteza kiimani.Pia kumbuka yya kwamba Mungu ndio dira yetu ukimpoteza utayumba na kuangamia,Usipoteze njaa na kiu mbele ya MUNGU wako ,usikate tama ewe mteule wa MUNGU.
ZAB 63:1 Ee MUNGU,MUNGU WANGU NITAKUTAFUTA MAPEMA NAFSI YANGU INAKUONEA KIU MWILI WANGU UNAKUONE SHAHUKU KATIKA NCHI KAME NA UCHOVU ISIYO NA MAJI.