Thursday, December 26, 2013

NASI TUMEKUJA KUMWABUDU.

MCH. EZEKIELI JOSEPH

ALIYE SHIKA BIBIIIA NI MAMA MCH. ANNA EZEKIELI AKIWA NA WANFUNZI WAKE,picha na makitaba
NASI TUMEKUJA KUMWABUDU.
NA OSCAR SAMBA.
Hakika ni siku nyingine tena iliyosheheni utukufu mkuu wa MUNGU wetu wa mbinguni,Kwa jina la BWANA wetu YESU KRISTO nina kukaribisha katika makala hii inayo zungumzia Kuzaliw akwa YESU pamoja vitu muhimu vinavyo ambatana na sikuu hiyo.
Ujumbe huu umetolewa jana madhabahuni katika kanisa la VICTORY CENTRE LA TAG lililopo hapa mkoani ARUSHA eneo la kwa MOROMBO na mwalimu EZEKIELI JOSEPH kutoka jijini DR ES-SALAAM,      
Bila kupoteza muda na tutazame maandiko; MATHAYO 2:1-12.
Mpendwa ukisoma maandiko hayo utaona Yesu alivyozaliwa katika bethilehemu ya uyagudi enzi za mfaulme Herode,,Ukiendela utaona jinsi mamajusi walivyo tazama nyota na kwenda kumuona YESU pia walimtolea zawadi nyingi.
Wengine wanafikiria ni wanawake kwa sababu wanaitwa mamajusi na wengine wanazani ni mijusi,,MAMA JUSI NI WINGI UMOJA NI MAJAS,ndini ya ZOROTEANISM ilianzishwa Iran kabla ya YESU ilikuwa ni dini kubwa ya WAHAMEDI na WAHEDENI ambao makuhani wao waliitwa hivyo.
Walikuwa wakisomea elimu za nyota na zakishirikina za kusoma nyota.
Chakushangaza ni kwanini MUNGU alijifunua kwa watu hawa ,Ila nimegundu haya kwamba MUNGU humtumia mtu yeyote,
MTHAYO 16:2-3 akajibu akawaambia kukiwa jioni mwasema Kutakuwa kianga kwa maana mbingu ni nyekundu,,,na asubuhi mwasema leo Kutakuwa na dhoruba kwa maana mbingu ni nyekundu,tena kumetanda.Enyi wanafiki mwajua kuutambua uso wa mbingu bali Ishara za zamani hamuwezi kuzitambua.
Manaeno haya YESU alikuwa akizungumza na watu wenye uwezo wa kutambua mambo kupitia sanyansi ya asili,ambayo ni miongoni mwa hizo elimu za kusoma nyota..Elimu hii ilikuwa sana kule mashariki ya kati, na baadae kuonekana  paka kwa wayahudi.
Wahubiri wengi hutumia andiko hilo kuhubiri mafundisho ya kusafisha nyota ila kibibilia mafundisho hayo hayapo; yanayo halalisha mahubiri hayo.
Habari ya kusafisha nyota ni mambo ya wanajimu nasio walokole,Mafundisho ya kusafisha nyota ni utapeli kama utapeli mwingine.
Torejee tena kwenye somo letu,Kusudi la safari yao (MAMAJUSI) ili kuwa ni kumwabudu MFALUME, kuabudu kwao kulifunua tabia tatu za mwabudu wa kweli.
1.FURAHA, MATHAYO 2:10, NAO WALIPO IONA ILE YOTA WALIFURAHI KWA FURAHA KUBWA.
Kuabudu ni jambo la furaha kwa mwabudu linalotokana na furaha ya kweli kwa MUNGU wake ,wito wetu wa kwanza ni kumwabudu MUNGU,katika kuabudu ndipo unaweza kuitwa MCHUNGAJI au MWINJILISITI….
Unapo mwabudu MUNGU kwa furaha unakutana na furaha yake pia furaha ya MUNGU ni nguvu tele.

 ZAB 16:11, UTANIJULISHA NJIA ZA UZIMA MBELE ZA USO WAKO ZIKO FURAHA TELE NA KATIKA MKONO WAKO  WA KUUME KUNA MEMA YA MILELE.
Kama adui atafanikiwa kuiba furaha yako basi amekwisha kukupokonya nguvu na ukishaishiwa nguvu ni dhairi ya kwamba umekwisha kushindwa.
2.HALI YA UNYEYEKEVU, Lilionekana pale walipo msujudia mototo mdogo
MATHAYO 2:11A. WAKAINGIA NYUMBANI WAKAMUONA MTOTO PAMOJA NA MAMAYE MARIAMU, WAKAANGUKA WAKAMSUJUDIA.
Unyenyekevu ni jambo la kiroho na linaanzia kwenye MOYO wa mtu,
MATHAYO 11:29-30  JITIENI NIRA YANGU MJIFUNZE KWANGU KWA KUWA MIMI NIMPOLE NA MNYEYEKEVU WA MOYO. KWA KUWA NIRA YANGU NI LAINI NA MZIGO WANNGU NI MWEPESI.
Nira ni ile ambayo wanaolima kwa kutumia ng’ombe huwafunga shingoni ila ile ni nzito na ni ngumu kwani huwachubua shingoni.Lakini YESU anasema ya kwake ni nyepesi na ni laini.
Kama hakuna unyenyekevu hakuna KUABUDU badala yake kuna mizaha ya kidini,Unyenyekevu ni maisha ya kiroho ya mwamini hakuna.Mambo ya kiroho ynahiytaji unyenyekevu mkubwa.
ISAYA 6. Ukisoma utamuona Isaya alivyo waona malaika walivyo kuwa wakimwabudu MUNGU na kufunika sura zao; kwa maana hiyo walitaka MUNGU aonekane nasio wao,mfano wapo wachungaji na wahubiri ambao hutaka waonekane wao kwanza nasio MUNGU.
Ukifanya mabo ya YESU iliwewe utukwizwe safari yako ya kiroho haitakuwa ndefu,
3.WALITOA, UTOAJI UNAENDANA NA KUABUDU,
MWANZO 2:5- IBRAHIMU AKAWAMBIA VIJANA WAKE KAENI HAPA NITAENDA NA KIJANA KUABUDU NA KUWARUDIA TENA, BASI IBRAHIMU AKAMTWIKA ….
Isaka alifundishwa kuabudu kwa njia ya kumtolea MUNGU,tuwafundishe watoto wetu kumtolea MUNGU. Wapo watu wanaohitaji kubarikiwa kama IBRAHIMU lakini hawahitaji kutembelea kwenye njia alizo tembelea IBRAHIMU,nisawa na kusubiri meli kwenye stendi ya ubungo jambo ambalo haliwezekani ila ukiisubiri bandarini inawezekana.
Kwa hiyo huwezi kubarikiwa bila kufwata kanuni .MUNGU wetu hafanyi kazi nje ya NENO,Watu wapo tayari kuoga uchi njia panda,kukaa kwenye makaburi usiku kucha na kula nyama za watu, ikiwa ni mashariti ya mganga wa kienyeji.
Ila kwa mambo ya rohoni watu hawako tayari kumtii MUNGU, kwa namna yoyote ile,kama kunamchawi wa kwanza katika maisha yako ni wewe mwenyewe fanya kile kitu ambacho MUNGU anataka ufanye,usipotoa hautafanikiwa; maisha yako yana hubiri kuliko maneno yako yenyewe.
Utoaji wa fungu la kumi hatutoi kama sheria toa kama upendo,wapo watu ambao saluni hutumia fedha nyingi lakini hutoa kidogo.Mtu yuko tayari kukaa saluni masaa saba ila mbele za MUNGU hakai masaa saba.Kusuka sio dhambi ila ni vizuri kuweka usawa.
Soma ..MALAKI 1:6-8  METHALI 3:9
Fedha ambazo unazizuia kwa MUNGU zitaenda sehemu nyingine.
Tutazame jinsi ambavyo MAMAJUSI WALIVYO MTOLEA MUNGU;
1.DHAHABU, ili kuwa ni zawadi ambazo wakipewa wafalume au watawala.Watu hawa walielewa nafasi ya YESU kama MFALUME.Ingawa watu hawa hawakuwa na ufahamu wa kutosha kwa MUNGU ila walitoa.
Unapo toa vitu vya dhamana kwa MUNGU unaonesha ni kwajinsi gani unavyo mjali,
2.UVUMBA, uvumba uliashiria kazi ya kikuhani (KUHANI MKUU) walikuwa wakivukisha sehemu ya PATAKATIFU-PAPATAKATIFU kwa maana nyingine walimtambua YESU kama KUHANI MKUU.MAKUHANI wa AGANO LA KALE ili kuwa ni kivuli cha YESU,UKUHANI wao haukuwapa kibali watu kuingia mbele za MUNGU ila UKUHANI wa YESU umetupa nafasi ya kuingia wote.Kwahiyo unaouwezo wa kenda mbele zake.
3.MANEMANE, manemane hili  ni dawa ya kuzikia miili ya watawala iliyogunduliwa miaka ya 300 kabuka ya KRISTO,zilipakwa ili wasioze.
Kwa maana nyingine zilitabiri kifo cha YESU,ndo maana baada ya kifo chake wanafunzi wake walipaka mwili wake manukato ambayo ndiyo manemane.
KUABUDU NITENDO LA UFUNUO.
YOHANA 4:24  MUNGU NI ROHO NAO WAMWABUDIYE YEYE YA WAPASA KUMWAMUDU KATIKA ROHO NA KWELI.
Zamani walikuwa wakiabudu katika sehemu mbalimbali na hapo walikuwa wakibishana na kuvutana katika sehemu ya kuabudu, kwa pamoja tusome..
EFESO 2:1  NANYI MLIKUWA WAFU KWA SABABU YA DHAMBI NA MAKOSA YENU.
Mtu kama hajaokoka ni mfu,kama mtu amekufa kiroho hawezi kuabudu,wengine wajua ya kwamba kuabudu ni kupiga magoti au kuimba nyimbo za polepole ila kuabudu ni UFUNUO WA ROHO YA MTU.Mafarisayo na Makuhani pia Waandishi walikosa huo ufunuo ingawaje waliyajua hayo yote.
Mpe YESU nafasi ya kwanza moyoni mwako unapo mwabudu weka pembeni mabo yote elimu,cheo au fedha.MAMAJUSI MUNGU aliwapa UFUNUO wa kipekee ambao uliwafanya wa MTAMBUE YESU KAMA MFALUME.
Kuabudu ni maisha yako ya kila siku, hakikisha unaishi maisha ya ibada,wapo watu ambao kanisani wanongea ila nyumbni haongei huo ni usanii wa wakaida haya ni maonesho ya kidini  na mizagha,Ibada ni mfumo wa maisha yetu kinyume cha hapo ni USANII.
Tengeneza kila wakati,YAKOBO aliwakaja watu  kuacha makorokoro yote ili waka MWABUDU MUNGU.Kila unalolitenda hakikisha ni jema,Kabla ya kuusogelea utukufu wa MUNGU.
YESU AZALIWE KWENYE MOYO WAKO.
MATHYO 15:18-19
MIMI nimeokoka na ninampenda YESU WEWE JE?
Kama bado basi ungana nami kwenye sala hii kisha utaokoka kumbuka kuokoka sio dini mpya bali ni mwanzo mpya na MUNGU WETU ALIYE MBINGUNI , tuanze sasa;
“Ee MUNGU WANGU ULIYE MBINGUNI MIMI NI MWENYYE DHAMBI NA MIMESIKIA HABARI ZAKO NA KUZIAMINI EWE YESU NI SAFISHE KWADAMU YAKO NA UNIKOWE”
www.bereacc.blogspot.com

No comments:

Post a Comment